MAHABUSU AFARIKI DUNIA BAADA YA KUJINYONGA KWA KUTUMIA TAMBARA LA KUPIGIA DEKI KWENYE CHOO CHA MAHABUSU MBEYA



MAHABUSU, Vumi Elias (30), amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia tambara la kupigia deki ndani ya choo cha mahabusu ya Kituo cha Polisi Tunduma.
 
Elias, mkazi wa Maporomoko-Tunduma, aliyetuhumiwa kwa unyang’anyi wa kutumia nguvu katika eneo la Tunduma wilayani Momba, alifariki dunia jana, saa 12 asubuhi muda mfupi baada ya kufikishwa katika Kituo cha Afya Tunduma kwa matibabu.
 
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Robert Mayala, alisema Elias aliingia choo cha mahabusu saa 10 alfajiri na kufanya jaribio la kujinyonga kwa kutumia nguo ya kupigia deki.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo