Klabu ya nyimbo za injili iliyofunguliwa jijini Dar es Salaam
Dar es Salaam.
-------
Imezoeleka
kuwa klabu za usiku zimekuwa zikitumika kwa mambo ya starehe huku
viongozi wa dini wakizichukulia kama maeneo hatari kwa waumini wao.
Tofauti
na maeneo mengine ya starehe, klabu za usiku huwa na kumbi za muziki
zenye taa za kumweka za rangi mbalimbali huku giza likitawala na wakati
huo huo muziki hupigwa kwa sauti ya juu.
Mbali
na muziki, klabu hizo husheheni vileo vya kila aina huku watu
wakiruhusiwa kuingia na mavazi yoyote wakiwemo wale wanaopenda kuvaa
nuzu uchi.
Hata hivyo kwa watumishi wengine wa Mungu, klabu sasa ndiyo pamekuwa mahali pa kuvunia waumini.
Mchungaji
Harris Kapiga wa kanisa la Nchi ya Ahadi lililoko Sinza Kamanyola,
ameamua kuanzisha klabu ya usiku kama zilivyo klabu nyingine za starehe.
Klabu hiyo iliyozinduliwa hivi karibuni maeneo ya Mbezi Tangibovu katika hoteli inayoitwa Mak Hotel, imeonekana kuvutia vijana wengi ambao walionekana wakifurahia mandhari na muziki uliokuwa ukipigwa ndani yake.
Tofauti
na klabu nyinginezo, Mchungaji Kapiga anasema kutakuwa na udhibiti wa
vishawishi vya dhambi ikiwa pamoja na ulevi, mavazi yasiyo na staha na
aina ya muziki unaopigwa.
Anasema tangu alipoanzisha wazo hilo, watu wengi hasa wachungaji walikuwa na wasiwasi kuhusu vishawishi hivyo.
“Tangu
nimeanza wazo langu hili nimekumbana na vikwazo vingi. Imeshtua watu
wengi, japo wengi wamelikubali na kuna baadhi hawakubali ila hawawezi
kusema wazi,” anasema na kuongeza:
“Wengine
wanajiuliza nitawezaje kudhibiti vipi hali ya klabu kwa sababu maeneo
haya kunakuwa na anasa, ulevi na masuala ya mavazi watu watavaaje, na
mimi nawajibu.”
“Mtu
akija hapa na mavazi mabaya hataingia, tutakuwa makini sana katika
hili. Mtu avae nguo yenye staha, siyo mtu aje nusu uchi, tutamtoa kwa
nia njema tu. Hata mtu aliyelewa tutamtoa labda tusimgundue.”
Kwa
nini ameanzisha klabu ya usiku? Mchungaji Kapiga anasema alianza kupata
wazo hilo siku alipokuwa kwenye sherehe za kuadhimisha kuzaliwa kwa
Clouds Media ambako pia ameajiriwa kama mtangazaji
Credit-Skendo za mjini