skip to main |
skip to sidebar
DK.CHENI AIKUMBUKA KAOLE, AAPA KUIRUDISHA!
Stori: Shani Ramadhani
MWENYEKITI Msaidizi wa
Bongo Movie Unity, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ amesema amekumbuka na
kutamani kurudisha Kundi la Sanaa ya Maigizo la Kaole ‘Kaole Sanaa
Group’ liwe na nguvu kama zamani.
Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’.]
Dk. Cheni alisema japo kundi hilo limeonekana kupoteza mvuto wake wa
awali, lakini anaamini wasanii wengi wanaofanya vizuri kwenye tasnia ya
filamu kwa sasa wametoka katika kundi hilo maarufu.
Hata hivyo, pamoja na kupotea kwa kundi hilo, Dk. Cheni anatamani
sana kulirejesha kwenye ulingo wa sanaa na kwamba kuna mikakati
anayoiandaa ili kukamilisha azimia hiyo.
“Naitamani Kaole ya zamani, nahisi kama kuna vionjo vinakosekana siku
hizi. Wasanii wengi wenye majina makubwa kwa sasa wametoka kwenye kundi
hilo, lakini nitajitahidi kulirudisha, naamini nitafanikiwa,” alisema
Dk. Cheni.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi