DIWANI HAILE NYUMA MWENYE SUTI NYUMA AKITOKA MAHAKAMANI

ASKARI MAHAKAMANI

DIWANI
wa Kata ya Kitaji Manispaa ya Musoma Haile Tarai (Chadema) pamoja
nawatu wengine watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa
wa wakidaiwa kumfanyia fujo Mjumbe wa Halimashauri Kuu ya CCM(NEC)
Vedastus Mathayo katika msiba wa Shekh wa mkoa wa Mara Athumani Magee.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Faisal Kahamba,imedaiwa na mwendesha mashitaka wa polisi Jonas Kaijage mnamo January 30 mwaka huu watu hao walimsababishia usumbufu na fujo ambazo zingeweza kuhatarisha amani miongoni mwa jamii wakati Mathayo akiwa ndani ya gari aliyokuwa akiendesha mwenyewe kuelekea kuhani msiba.
Washitakiwa hao walidaiwa kutenda kosa hilo kinyume na kanuni ya adhabu kifungu cha 171(a) sura ya 16 ya mwaka 2002 na kufunguliwa kesi namba 31 ya mwaka 2014