CCM YATOA SHUKRANI KWA WANANCHI KUIMWAGA CHADEMA KATIKA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI ULIOFANYIKA JANA


 
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza  na waandishi wa habari leo.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewashukuru Watanzania kwa kukiamini na kukipatia ushindi wa kishindo katika uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika jana katika kata 27 na CCM kushinda kata 23.

Akitoa shukrani hizo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema leo kwamba siri ya CCM kuimwaga CHADEMA ni uadilifu katika kuwatumikia wananchi na kwamba, kushindwa kwa chama hicho ni ushahidi kwamba hakikubaliki na Watanzania wamewathibitishia kwamba hawajazoea vurugu.

Nape alisema CCM inaahidi kuendelea kuwatumikia Watanzania kwa amani na utulivu kwa kuwa ina uzoefu wa kufanya siasa kistaarabu na ndio siri ya kukubalika kwa wananchi.

Akizungumzia kushindwa kwa CHADEMA alisema wamehukumiwa kutokana na vurugu na kupiga watu kwenye kampeni za uchaguzi na ndio maana wametumia gharama kubwa na helkopta tatu na kuambulia kata tatu.

"CHADEMA wamevuna walichopanda Watanzania hawapendi vurugu, wamezoea amani na utulivu sasa wamewaadhibu kwa kuwanyima kura na huo ni ushahidi kwamba Watanzania hawakiamini," alisema.

Katika uchaguzi huo CCM  ilishinda katika kata 23 za Kibindu na Magomeni (Pwani), Kiwalala na Namikage (Lindi), Ubwage (Shinyanga), Ibumu na  Nduli (Iringa), Kiomoni na Mtae (Tanga), Nyasura(Mara), Malindo, Santillya (Mbeya), Partimbo(Arusha, Mkwiti (Mtwara), Tungi na Ludewa (Morogoro) na Mrijo (Dodoma).


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo