BREAKING NEWSS: CCM WASHINDA KWA KISHINDO KATA ZOTE TATU MKOA WA IRINGA

 Wafuasi wa CCM Iringa  wakimpongeza kaimu katibu  wa CCM mkoa wa Iringa Hassan Mtenga kwa kufanikisha  chama  hicho kushinda  uchaguzi mdogo kata ya  Nduli kama alivyopata  kumuahidi mbunge wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa  (Chadema) katika mikutano yake kuwa safari ya kumng'oa ubunge 2015 itaanzia katika uchaguzi huo mdogo kata ya Nduli kuwa lazima Msigwa atake atatoa na asipo taka atatoa jimbo la Iringa mjini 
Wafuasi wa CCM kata ya Nduli  wakiwa  wamemnyanyua  juu  juu  aliyekuwa mgombea  udiwani kata ya Nduli Bw Mtove  baada ya  matokeo kumpa ushindi wa kishindo leo 
=========
CHAMA  cha  mapinduzi (CCM)  mkoa  wa  Iringa  kimefanikiwa  kutetea kata  zake  zote tatu ambazo  leo   wananchi  wameshiriki  kupiga kura  kuwachagua madiwani  kufuatia nafasi hiyo kuwa wazi baada ya madiwani wake kufariki  dunia  huku chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) kikishindwa  vibaya katika  uchaguzi huo.

Mbunge  wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (Chadema) ambae  alikuwepo  eneo la Nduli  akifuatilia  matokeo  ya uchaguzi huo pamoja na  wafuasi wa Chadema  alilazimika  kuondoka katika eneo hilo  baada ya  kubaini kuwa hali ya ushindi kwa Chadema ni ndoto.
 
Huku   wafuasia  wa  CCM  wakionekana  kumpongeza  aliyekuwa mgombea wa CCM kata ya Nduli pamoja na  kaimu katibu wa CCM mkoa wa Iringa  Hassan Mtenga kuwa  kazi  yake imeonyesha inaonyesha  wazi  safari yake ya  kulitwaa jimbo la Iringa mjini .


Katika  Matokeo hayo ambayo hadi sasa  majira ya saa 12.50  bado msimamizi wa uchaguzi kutangaza CCM inaongoza kwa kura 810 huku  Chadema  wakifuatia kwa kura 491
Mbali ya  matokeo  hayo ya kata ya  Nduli pia  CCM imeshinda kata ya Ibumi na Ukumbi zote za  wilaya ya  Kilolo.
 
na Francis Godwin


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo