MWIMBAJI mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Ramadhan Masanja ‘Banza
Stone’ amefunguka mazito juu ya matumizi mabaya ya bangi na madawa ya
kulevya ikiwa ni pamoja na jinsi alivyokuwa akiyatumia.
Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ kabla ya kufanya mahojiano na Global TV Online.
Akizungumza kupitia Kipindi cha Mtu Kati cha Global TV Online
mwanzoni mwa wiki hii, Banza alikiri kutumia madawa ya kulevya na
kusema; “Nilianza kuvuta sigara ya kawaida, nikaja bangi na baadaye
madawa ya kulevya aina ya Heroin ambapo alikuwa akiyatumia kwa
kuchanganya na sigara au bangi.
“Ujana
ulisababisha nikajiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya ila sasa
nimeacha kabisa na nawashauri vijana wenzangu kuwa mbali na kilevi
hicho kwani kama huna kipato cha kutosha unaweza kugeuka kibaka maana
mwili ukizoea ni vigumu kuacha.”
CHANZO; Global Online TV
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi