Afande Sele ameungana na Rais wa Marekani Barack Obama katika
kuunga mkono kauli yake ya kwamba bangi ni salama kuliko pombe kwa afya
ya binadamu
Akiongea na kipindi cha
Milazo XP kinachorushwa na TBC fm, Afande Selle, mbali na kuunga mkono
pia alizungumzia umuhimu wa bangi kama zao linaloweza pia kuwa na
manufaa kwa uchumi wa nchi kama litatumiwa kwa usahihi.
