Kamanda
wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaama Suleiman Kova ameongea na
Waandishi wa Habari na kutoa tamko kama Jeshi la Polisi Nchini kuhusiana
na kutekwa kwa Mwnyekiti wa Chadema Wilaya ya Temeke Joseph Yona,hivi
ndivyo alivyoanza kuongea na waandishi
‘Katika
tukio la kutekwa nyara Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Temeke anayeitwa
Joseph Yona ni kwamba tumeamua kufatilia kwa makini matukio kama haya
lakini habari kwa ufupi ni kwamba huyo mlalamikaji Joseph Yona alitoa
taarifa za kutekwa kwake na baadae kutupwa vichakani kule eneo la Ununio
kwa mlinzi ambae alikua kwenye kazi zake za kawaida’
‘kinachoonekana pale kwa uchunguzi wa awali huyu mlalamikaji alikua
anapata vinywaji kule Temeke katika Grocery iitwayo Mgumbini walifika
watu 6 kwanza walijitambulisha kama maafisa polisi lakini yeye
akamtambua mmoja wapo kuwa si Afisa Polisi hiyo ilikua saa 5 usiku’
‘Wakamwambia wanataka kumpeleka kituo cha polisi hawakumueleza kosa
walimwambia twende kituo cha polisi sisi ni askari polisi lakini yeye
akauliza kwamba kati ya nyinyi sita mbona huyu mmoja namfahamu kwa sura
na jina na mwanachama mwenzangu wa Chadema na tunafanya nae kazi kila
siku mnasemaje nyie wote maafisa wa polisi’
‘Aliposema hivyo wale wakakasirika wakamnyakua haraka wakamuingiza
kwenye Gari aina ya Landcruiser wakachukua kitamabaa wakamfunika usoni
ili asiendelee kuwaona tena huku wanamhoji katika mahojiano yao ndani ya
gari’
‘Kutokana na maelezo ya mlalamikaji walikua wanamhoji kwa nini
anaendelea kumuunga mkono au kumshabikia Zitto Kabwe wa Chadema na vile
vile walikuwa wanataka wamuonyeshe rafiki yake ambaye nae ni mwanachama
wa Chadema kwamba nae apatikane haraka sasa huyo mlalamikaji hakuwapa
ushirikiano wa kumuonyesha rafiki yake huyo mwingine ambae nae ni
mwanachama wa Chadema’
‘kwa hiyo walichokifanya sasa wakaanza kumpiga huku wakimuhoji
masuala mbalimbali mpaka alipopoteza fahamu na alipigwa zaidi alipohoji
mnasema mannanipeleka Central mbona hatufiki Kwa hiyo tukio hili moja
kwa moja ni tukio la utekaji nyara ambalo ni kosa kubwa sana katika nchi
yoyote ukiachilia mbali Tanzania’
‘Sisi tunasema hivi nimeunda jopo la wapelelezi chini ya Mkuu wa
Upelelezi kanda maalum Japhary Mohamed na assistant commissioner ambao
nimewapa maagizo wafanye upelelezi wa haraka mno na bahati nzuri
mlalamikaji ana ushirikiano mzuri na ana akili zake hao watuhumiwa
nimesema wapatikane haraka kwa speed kali kadri inavyowezekana ili hatua
kali za kiseria ziweze kuchukuliwa’
‘Kutokana na tukio kama hili natoa onyo kali Mtu yoyote au hasa
kikundi kiwe cha dini cha siasa au chochote kile wanapokuwa na mgogoro
ni vizuri zaidi wakafata mkondo wa kisheria badala ya kufanya
fujo,vurugu,utekaji nyara hii haisadii chochote katika kutatua migogoro’
‘Fuata taratibu za kisheria kuna mahakama kuna mabaraza mengi ya
usuluhishi kuna wazee kwenye makundi au vyama kwa sababu tukiacha hivi
ikaendelea hivi tutaambukizana katika makund mengine na wale
watakaopatikana wajielewe kabisa kwamba watachukuliwa hatua kali sana
za kisheria’
‘Kwa sababu inaonekana ni watu wanaofahamika ushauri wangu wa bure ni
bora wajisalimishe kwa sababu hakuna kilichojificha yule mlalamikaji
baadhi ya watu anawafahamu kwa hiyo ni bora wajisalimishe wenyewe kwa
sababu hata wasipojisalimisha sisi tuna uwezo wa kuwakamata sasa
ukikamatwa bila kujisalimisha kuna utofauti na pale ulipojisalimisha
mwenyewe maana angalau utakua umeonyesha ushirikiano’
‘Katika tukio hili hatutofanya ajizi hakuna atakaesalimika kwa wale
watakaokuwa wamehusika katika tukio hili hatutojali nafasi gani unayo
katika jamii,yoyote yule atakae tajwa kwa namna moja au nyingine
alishiriki,alichochea au alipanga wote wale watakamatwa watashughulikia
ili kuondoa huu mtandao wa utekaji nyara
‘Nchi yetu ni nchi ya amani hatupendi vitu vya utekaji nyara ni
tishio kubwa kwa usalama wa wananchi wa kawaida na hatawatu wengine
wenye nafasi tofauti’.
