BREAKING NEWS: MADEREVA WA MALORI WAFUNGA BARABARA TABORA


Taarifa iliyotufikia asubuhi hii inasema malori zaidi ya 40 yamezuia njia kufuatia tukio la kutekwa kwa madereva wenzao watatu wa malori na majambazi kisha kukatwa mapanga,na inasemekana baada ya tukio hilo kutokea polisi walichelewa kufika eneo la tukio. IMG-20140126-WA0003Mbali na malori kuna mabus ya abiria na magari binafsi ambayo nayo hayawezi kupita kufuatia agizo la madereva hao ambalo wamesema hawaachii njia mpaka Mkuu wa Mkoa wa Tabora au Rpc  afike,huku wakidai hilo limekua ni tatizo sugu eneo hilo kutokana na kutokea vitendo vya utekaji mara kwa mara.
IMG-20140126-WA0006Eneo hili linaitwa laziba lipo katikati ya mji wa Laziba na Nzega,ni kilomita 20 kutoka Nzega Mjini,madereva hao wa malori wameziba njia tangu saa 3 asubuhi hii,japo taarifa inasema tukio la kutekwa kwa madereva hao limetokea jana  saa 3 usiku.

CHANZO; MILLARD AYO.COM


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo