MAMA SALMA KIKWETE APOKEA TUZO KUTOKA KITUO CHA MAENDELEO YA KIUCHUMI NA UONGOZI (CELD)

 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake  na Maendeleo, WAMA, Mheshimiwa Mama Salma Kikwete akipokea tuzo ya Uongozi Uliotukuka kimataifa (Global Inspirational Leadership Award 2013) kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Maendeleo ya  Kiuchumi na Uongozi Mheshimiwa Bibi Furo Giami, mwishoni mwa mkutano wa siku tatu wa Wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia.  Mkutano huo ulioandaliwa na Kituo cha Maendeleo ya Kiuchumi na Uongozi  (CELD), wakishirikiana na CEO Clubs Network na African Leadership Magazine uliofanyika katika hoteli ya Atlantis The Palm, huko Dubai , Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE.) Tuzo hiyo imetolewa tarehe 18.12.2013.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba ya kushukuru mara tu baada ya kupokea Tuzo hiyo huko Dubai
 Mkurugenzi  Mtendaji  wa Kituo cha Maendeleo ya Kiuchumi na Uongozi (CELD), Bibi Furo Giami akikabidhi vyeti kwa Wake wa Marais na wanawake wengine waliotunukiwa tuzo hizo wakati wa kilele cha mkutano wa wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia uliofanyika huko Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu
 Dr. Angela Moore, Balozi wa Hisani kutoka kutoka Jimbo la Georgia, nchini Marekani akiwavisha nishani washindi wa Tuzo .
 Wake wa Marais kutoka Barani Afrika waliotunukiwa Tuzo na Kituo cha Maendeleo ya Kiuchumi na Uongozi wakionyesha tuzo,nishani na hati walizokabidhiwa kwa washiriki wa mkutano wa wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia na wageni wengine waliohudhuria sherehe ya utoaji tuzo hizo huko Dubai
 Wake wa Marais kutoka Barani Afrika waliotunukiwa Tuzo na Kituo cha Maendeleo ya Kiuchumi na Uongozi wakionyesha tuzo,nishani na hati walizokabidhiwa kwa washiriki wa mkutano wa wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia na wageni wengine waliohudhuria sherehe ya utoaji tuzo hizo huko Dubai.Picha na John Lukuwi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo