KAGAME ATOA KALI YA MWAKA, AFIKA AFRIKA KUSINI KUUAGA MWILI WA MANDELA NA KUONDOKA SAA HIYO HIYO

KATIKA hali isiyotarajiwa, Rais Paul Kagame wa Rwanda Jumatano iliyopita aliwashangaza wengi baada ya kufika ghafla jijini Pretoria, Afrika Kusini na kuaga mwili Mzee Nelson Mandela na kuondoka mara moja.

Pamoja na kuwasili ghafla bila taarifa Pretoria, Kagame alikwenda moja kwa moja katika majengo ya Union Buildings na kwenda kuaga mwili huo kisha alielekea uwanja wa ndege na kuondoka.


Habari ambazo Rai Jumatano imethibitisha zinasema aliondoka saa chache baada ya kuuaga m
wili wa shujaa Mandela na kuelekea Rwanda ambako alikwenda kuongoza Mkutano Mkuu wa chama tawala cha Rwanda Patriotic Front (RPF), ambapo alichaguliwa kuwa Mwenyekiti.

Habari za ndani zimesema kuwa Kagame ambaye alikuwa na ulinzi mkali, aligoma kwenda kusalimiana na mwenyeji wake Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini.

Kuja ghafla kwa Kagame na Rais Omar al Bashir wa Sudan katika kumuaga Mandela kulizua maswali mengi, kwa vile Rwanda ilitangaza kuwa Rais Kagame hatahudhuria mazishi hayo na badala yake itatuma ujumbe wa viongozi wa juu wa nchi hiyo nchini Afrika Kusini.

Serikali ya Afrika Kusini awali ilitangaza kuwa Waziri Mkuu wa Rwanda, Pierre Habumuremyi, Katibu Mkuu wa RPF Francois Ngarambe, ndio wangeongoza ujumbe wa nchi hiyo katika mazishi hayo.

Clyson Monyela, Naibu Mkurugenzi Mkuu na Msemaji wa Wizara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Mahusiano ameliambia Rai Jumatano jana kuwa Serikali awali ilipokea jina la Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wa RPF, lakini baadaye waliambiwa kuwa Kagame amewasili mwenyewe na ujumbe wa watu wachache.

Monyela alisema walipokea orodha ya maraisi wengi wa Afrika wakiwamo kutoka Kenya, Uganda, Congo DRC na Burundi lakini hawakupokea jina la Kagame ingawa alitokea ghafla na wala hakwenda kumpa pole Zuma, ila alituma ujumbe kwa Rais Zuma na wananchi wa Afrika Kusini.

“Hatukupokea jina la Rais Kagame kwa vile Serikali ya Afrika Kusini haina tabia ya kumualika mtu kwenye msiba wala mazishi, hiyo ni tabia ya wananchi wa nchi hii,” alisema.

Msemaji huyo alisema kuwa hakuna hata Rais au kiongozi yoyote aliyealikwa katika msiba na mazishi hayo, na ilikua ni utashi wa kiongozi kuthibitisha kuwa atahudhuria.

Rais Kagame katika muda wa hivi karibu amekuwa na ugomvi wa chini chini na maraisi Zuma, Kikwete na Banda kutokana nchi hizo wanachama wa jumuiya . . . .

BOFYA HAPO KUSOMA ZAIDI ----> http://bit.ly/1epNdRi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo