WATENDAJI WOTE SERIKALINI KUPIMWA NA MPANGO WA MABADILIKO MAKUBWA SASA (BRN)

Makamu wa Rais Dkt Mohammed Gharib Bilal amesema serikali itatumia mafanikio ya utekelezaji wa mpango wa maendeleo makubwa sasa BRN kama kigezo muhimu cha kupimwa kwa uwajibikaji wa mawaziri na watendaji wa idara za serikali.

Amesema katika kuwabaini viongozi wazembe wanaokwamisha jitihada za serikali , ofisi yake na ile ya Waziri Mkuu zinakusudia kushirikisha wananchi kufanya tathimini ya mafanikio ya utekelezaji wa mpango huo kwa kuweka wazi vigezo pamoja na matokeo ya upimaji.

Akifungua mkutano wa siku tatu wa majadiliano ya wiki ya sera za kuondoa umaskini unaofanyika Jijini Dar es Salaam Dkt Bilal amesema hatua ya kutumia vigezo vya upimwaji utasaidi kuimarisha uwajibikaji wa mawaziri na watendaji kwa viongozi na wananchi kwa ujumla.

Amesema dhima ya utekeleaji wa mpango wa matokeo makubwa sasa si kwa ajili ya serikali pekee bali unategemea muungano kati ya serikali na wananchi kama muhimili katika kufanikisha mpango huo.

Sanjari hilo pia amewataka wadau kutumia fursa zilizopo katika kuleta tija kwa vijana na wanawake ambao kwa kiasi kikubwa wanakabiliwa na umaskini.

Saad Sulum ni Naibu Waziri wa fedha anazungumzia mafaniko ya mkutano huo katika kufanikisha mapinduzi ya kiuchumi kwa kuangalia sera zilizopo.

Wachambuzi wa masuala ya kiuchumi walizungumza juu ya kile wanachokiona katika taswira nzima ya hali ya umaskini nchini.

Ripoti iliyotolewa katika mkutano kwa mwaka 2011 hadi 2012 inaonesha kuwa Mkoa wa Dar es Salaam unakabiliwa na umaskini kwa asilimia 0. 8 ambapo maeneo ya mijini ni asilimia 5.5, huku maeneo ya vijiji hali ya umaskini imebainishwa kuwa ni 7.9 na kauli mbiu ya mwaka huu ni kupanua wigo katika kutumia mifano bora na fursa zilizopo kwa maendeleo endelevu yenye kunufaisha watu wengi walio maskini.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo