Na Saimeni Mgalula,Mbeya
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba Mkoani hapo,wamepokea kwa mtazamo Tofauti waraka wa kusitisha ziara za kugagua miradi ya maendeleo uliotolewa na katibu wa tawala Mkoani hapa.
Akizungumza katika kikao cha madiwani wa Halmashauri hiyo kilicho fanyika mjini Chitete mwishoni mwa juma,kwamba waraka huo unapingana na agizo la waziri mkuu Mizengo Pinda alilotoa kwenye kikao cha ALAT Taifa kuwaruhusu madiwani kukagua mradi.
Ivyaranji Solemba Diwani viti maalumu wa kata ya masangano alisema ingekuwa Vizuri wilaya mpya zikapatiwa nafasi hizo hiyo kwasababu bado halmashauri hizo hazija jua miradi yao na jinsi inavyo kwenda
Naye Diwani wa kata ya Chiwezi Emmanuel Punte alisema miradi mingi wanayo taka kuitembela ni ile ambayo inatekelezwa chini ya Halmashauri mama ya Mbozi ambayo ndiyo iliyokuwa inasimamia miradi hiyo.
Aidha Diwani huyo alisema "kwa kuwa kulikuwa na fungu la Fedha lililoandaliwa kwa ajili ya Ziara za Madiwani kukagua miradi baada ya kusitishwa ziara hiyo fungu hilo linakwenda wapi?" alihoji
Afisa Utumishi wa Halmashauri hiyo Amilly Mfugale akitoa muongozo kwa Madiwani alisema kuwa Serikali inafanya kwa Taratibu za sheria na kanuni, hivyo pamoja na kuwa Waziri mkuu alikisharidhia ndiyo maana alitoa agizo hadi hapo waraka utakapofika.
Aliendelea kwa kusema kuwa madiwani hao hawataweza kuendelea na ziara ya kutembelea miradi mara tu waraka kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu utakapo wasilishwa kwa ajili ya utekelezaji na si vinginevyo.
Akijibu hoja za madiwani Kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo Juma Kitabuge alisema kuwa waraka huo hauja wazuia madiwani kupitia kamati ya Fedha na mipango itaendelea kukagua miradi hiyo hadi hapo itakapofika mamlaka hizo wilayani hapa,

Miongoni
mwa wilaya mpya 19 zilizo anzishwa hivi karibuni na Serikali ya
Muungano wa Tanzania kwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi ni pamoja
na Momba.