UFOO SARO ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI, AAPA KIAPO CHA SIRI AKIWA KITANDANI

Ufoo Saro akiwa hospitali baada ya kupigwa risasi na mzazi mwenzake, marehemu Anther Mushi.
SIKU chache baada ya Mtangazaji wa Runinga ya ITV, Ufoo Saro kuruhusiwa hospitalini alipokuwa amelazwa baada ya kudaiwa kupigwa risasi na mzazi mwenzake, marehemu Anther Mushi, ameibuka na kula kiapo cha siri.
  
Ufoo ambaye alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, katika tukio la yeye kupigwa risasi, alimpoteza mama yake mzazi aitwaye Anastazia Saro…
Stori:Brighton Masalu na Chande Abdallah
SIKU chache baada ya Mtangazaji wa Runinga ya ITV, Ufoo Saro kuruhusiwa hospitalini alipokuwa amelazwa baada ya kudaiwa kupigwa risasi na mzazi mwenzake, marehemu Anther Mushi, ameibuka na kula kiapo cha siri.
 
Ufoo Saro akiwa hospitali baada ya kupigwa risasi na mzazi mwenzake, marehemu Anther Mushi.
 
Ufoo ambaye alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, katika tukio la yeye kupigwa risasi, alimpoteza mama yake mzazi aitwaye Anastazia Saro aliyedaiwa kuuawa na marehemu Mushi aliyejiua kwa risasi.
 
Akizungumza na gazeti hili Ufoo alisema, kamwe hawezi kusema kilichokuwa kikiwagombanisha yeye na marehemu Mushi mpaka siku ya mwisho wa uhai wake.
http://api.ning.com/files/l8tah2vExAULAoDSzOz1POhNbFKkIlgOZXJ4VWhoq1BOrsbduXn5KOa8PS-UMuYpB5x9hzTnqBWYoqUT4vf-HOtIG9zyEfL3/UFOOSARO1.jpg?width=404
Ufoo Saro.
“Siwezi kuzungumzia kabisa chanzo wala ugomvi wetu mimi na marehemu Mushi. Hiyo itakuwa siri yangu,” alisema Ufoo.
 
Katika mahojiano na gazeti hili, mtangazaji huyo alipoulizwa kuhusu msimamo wake wa uhusiano baada ya kupona kabisa alisema, hawezi kujiingiza tena kwenye mapenzi kwa sasa.
 
“Sitaki kabisa kusikia juu ya mapenzi, siwezi kuliweka suala hilo akilini tena,” alijibu kwa kifupi kwa sauti ya chini lakini yenye mkazo.
GPL


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo