Afisa Lishe Mwandamizi toka Taasisi ya
Chakula na Lishe Bi. Maria Msangi akieleza kwa waandishi wa Habari (hawapo
pichani) kuhusu utekelezaji wa mpango wa uongezaji wa virutubisho kwenye
vyakula ili kusaidia kuondoa magonjwa yanayosababishwa na upungufu wa
lishe,wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya
Habari(MAELEZO).Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sayansi wa Taasisi hiyo
Dkt. Elifatio Towo.Picha
na Hassan Silayo-MAELEZO.
========== ======== =======
Na Georgina
Misama-MAELEZO.
Taasisi ya Chaula na Lishe yaiasa
jamii kuzingatia lishe bora kuanzia
kipindi cha ujauzito hadi mtoto anapofikisha miaka miwili.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi
Idara ya Sayansi ya Chakula na Lishe (TFNC) Dkt Elifatio Towo wakati wa mkutano
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Dkt
Towo alisema kuwa uzingatiaji wa lishe bora utachangia katika kutokomeza
utapiamlo na kuimarisha afya ya mtoto tangu akiwa tumboni kwa mama na kudumu
kwa maisha yake yote. “Watoto waliopata lishe ya kutosha na hasa katika
kipindicha siku 1000 za mwanzo tangu mama anapokuwa mjamzito mpaka mtoto
anapofikisha miaka 2 wanakuwa wamepata faida zitakazodumu katika maisha yao
yote” alisema Dkt Towo.
Aidha aliongeza kuwa uongezaji wa Vitamini
na Madini kwenye vyakula ni muhimu
katika utendaji kazi wa mwili kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 5 na
wanawake walio katika umri wa kubeba
mimba. Alifafanua kuwa tafiti zinaonesha kuwa asilimia 59 ya watoto chini ya umri wa miaka
5, na asilimia 41 ya kina mama wana upungufu wa madini chuma yanayopelekea
kushusha kiwango cha utengenezaji damu.
Akieleza namna ya kukabiliana na tatizo hilo,
Dkt Towo alisema kuwa, Taasisi imeanzisha
teknolojia ya uongezaji wa vitamin na madini katika vyakula vikuu kama
vile unga wa ngano, sukarik mafuta ya kula, na unga wa mahindi.
Akijibu swali la mwandishi alietaka
ujua licha ya kuwepo kwa vyakula mbalimbali kwanini baadhi ya watoto
wanaandamwa na magojwa, Afisa Mwandamizi wa Sayansi ya Lishe Maria Msangi
alisema kwamba lishe duni inasababisha kinga hafifu na kupelekea jamii yenye kuandamwa na
magonjwa hasa ya kuambukizwa. Uzinduzi wa Mpango kuongeza
virutubishi kwenye vyakula ulifanywa na
Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na tayari
vyakula hivyo vinapatikana kwenye maduka na sokoni vikiwa na nembo maalum
inayoonyesha vyakula hivyo vimeongezwa virutubisho.
