Serikali imepiga
marufuku wananchi kufanya shughuli zote za kibinadamu pembezoni mwa
hifadhi zaareli ikiwemo kujenga nyumba, kulima au kufanya biashara na
kuagiza watu wote ambao wanajihusisha na shughuli hizo kuondoka haraka
iwezekanavyo katika maeneo hayo ili kuepusha uharibifu wa reli na
madaraja unaochangiwa watu hao na kulisababishia taifa hasara kumbwa.
Kauli
hiyo ya saerikali inatolewa na naibu waziri wa uchukuzi Mhe Charles
Tizeba wakati akifanya ziara ya kutembelea madaraja ya treni yaliyopo
wilayani Bahi mkoani Dodoma ambapo amesema shuguliza kubinadamu
zinazofanyika pembezoni mwa hifadhi za reli zikiwemo kilimo na kupitisha
mifungo juu ya reli zinaweza kusababisha reli na madaraja kusombwa na
maji kipindi cha mvua.
