Na Miza Othman Maelezo -Zanzibar .
Makamu
wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi amezitaka Radio jamii kuandaa vipindi vya kuelimisha jamii husika
bila kuingiliwa na Chama chochote cha siasa au Taasisi nyengine ili
kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima katika kuendesha redio hizo.
Hayo
ameyasema huko Wilaya ndogo ya Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja wakati
wa uzinduzi wa Radio jamii ya kisiwa hicho ikiwa ni shaamra shamra za
kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 1964.
Amesema
Radio Jamii inatakiwa kuwa huru bila kuingiliwa na Tasisi za Serikali
na binafsi na zinatakiwa ziendeshwe na jamii wenyewe kwa manufaa
yao bila kuweka mbele maslahi ya kibiashara.
Amesema
iwapo Redio Jamii itatawaliwa na utashi wa kisiasa inaweza
kupoteza malengo yake katika utaarishaji wa vipindi na hatimaee
kusababisha kukosekana kwa amani katika sehemu husika na maeneo
mengine ya jirani vinavyopokea matangazo hayo.
“Naomba
mtambue kua chokochoko na fitna za kisiasa zikishamiri katika radio
yenu watu wa mwazo kuathirika ni nyinyi wenyewe”, aliwaeleza Balozi
Seif Ali Iddi.
Ameitaka Radio
Jamii ya Tumbatu kuandaa vipindi vitakavyoelekeza jamii ya kijiji
hicho mbinu za kujiajiri wenyewe kwa kutumia rasilimali iliyowazunguka
ya bahari, kutoa elimu kwa kinamama kufuata uzazi wa mpango na malezi
bora.
Aidha
amewataka wafanyakazi wa redio hiyo
kutaarisha vipindi vitakavyosaidia kutoa elimu za madras mbali mbali
pamoja na kuelimisha madhara ya uvuvi haramu, kulinda mazingira na
kuendeleza mila, desturi, silka na utamaduni wa wananchi wa Tumbatu
.
Balozi
Seif aliwataka wananchi wa Tumbatu kuitumia vizuri Radio hiyo kwa
maendeleo yao na kudumisha amani kwani vyombo vya habari vina mchango
mkubwa katika kuharakisha maendeleo na kuweka ustawi bora wa
wananchi iwapo itatumiwa vizuri.
Nae
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Pembe Juma Khamis amemuhakikishia
Makamu wa Pili wa Rais kwamba watahakikisha kuwa lengo la kuanzishwa
Radio hiyo linatimizwa ikiwa pamoja na kutoa mchango mkubwa wa
maendeleo ya wananchi wa Tumbatu na Mkoa wa Kaskazini kwa jumla.
Aidha
alilishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) kwa misada yake kwa Zanzibar ikiwa pamoja na
kufanikisha radio ya tatu ya Jamii Zanzibar ikitanguliwa na ile ya
Mtegani Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja na Micheweni kwa Pemba.
Akizungumza
katika uzinduzi wa kituo hicho, Waziri wa Habari, Utamaduni Utalii na
Michezo Saidi Ali Mbarouk amesema sekta ya Habari Zanzibari inaendelea
kupanuka na hivi sasa kuna vituo 20 vya Redio vinavyorusha matangazo
yake.
Amesema
baadhi ya vituo hivyo vinavyorusha matangazo ya masafa mafupi na
masafa ya mbali vimepatiwa vifaa vipya vya kisasa na vimeimarisha
utaarisha bora wa vipindi vyake.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
