RAY ATAJA SABABU ZA KUPENDA KUIGIZA MUVI ZA KIMAPENZI

Na Gladness Mallya, GPL
STAA wa filamu za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ ameeleza chanzo cha wasanii Bongo kuigiza mapenzi kwenye filamu ni kwa sababu Tanzania hakuna uhuru wa kuigiza.

Vincent Kigosi ‘Ray’.
Akizungumza hivi karibuni jijini Dar, Ray alisema msanii anapoonesha kipaji chake kwa kuigiza kitu kwa ajili ya kuelimisha jamii anarudishwa nyuma kwani wakati mwingine inafikia hatua ya filamu husika kufungiwa.

“Hapa Tanzania hakuna uhuru wa kuigiza kama zilivyo nchi nyingine ndiyo maana kila siku tunaigiza mapenzi tu. Niliwahi kutoa filamu ya Second Wife (Mke wa Pili), Waislam hawakunielewa mpaka baadaye.

Juzikati nilitaka kutoa filamu ya Sista Maria, Wakatoliki wameipinga isitoke, sasa nini kimebaki, ni kuigiza filamu za mapenzi tu,” aliema Ray.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo