PICHA:ASKARI WA OPARESHENI YA KUWASAKA MAJANGILI WAKIONGOZWA NA JESHI LA WANANCHI TANZANIA (JWTZ) LAWAMANI KWA KUCHOMA NYUMBA ZAIDI YA 600 ZA WANAKIJIJI


Hapa ndipo wanapoishi watu hawa baada ya nyumba zao kuchomwa moto
Watoto wakiwa michezoni huku wasijue watalala wapi ukifika usiku
Ni majonzi makubwa
Hizi ndizo nyumba zao , wanalala chini ya miti baada ya nyumba zao kuchomwa moto
Wakazi wa kijiji cha kabage wakihama kijiji hicho baada ya nyumba zao kuchomwa na askari waliokuwa wanafanya oparesheni ya kuwasaka majangili nyumba hizo zilichomwa wiki iliyopita kijijini hapo na kusababisha maelfu ya wanakijiji kuishi chini ya miti
Mzee na binti yake wakiwa wanaondoka wanaondoka
Wakina mama wakiwa wanafungasha
Wakubwa kwa watoto wakiwa wanakihama kijiji hicho
Wakiendelea kuhama kijijini hapo

Wakazi wa kijiji cha Kabage wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi wakiwa wanaishi chini ya miti na familia zao baada ya nyumba zao kuchomwa moto na askari waliokuwa wanafanya oparesheni majangiri wiki iliyopita jumla ya zaidi ya kaya 500 zilichomewa nyumba kijijini hapo na kuleta malalamiko ya wanakijiji hao kwa kile wanachodai kijiji hicho ni halali na kimesajiliwa kisheria toka mwaka jana na kupewa usajili wenye namba KT/KIJ/47
Hawana makazi tena hawa
Mtoto akiwa amelala huku akiwa hana pa kuhifadhiwa ikiwa nyumba yao imechomwa moto

Mchungaji wa kanisa la PAG wa kijiji cha Mwamkulu Petro Mahenga akimfariji mmoja wa wahanga waliochomewa nyumba zao katika kijiji cha kabage wilayani Mpanda Daudi Belehiwa ambae pia mke wake aitwae Kurwa Elias alijifungua mtoto ambae hajatimiza miezi yake kutokana na kutembea kwa muda mrefu wakati akiwakimbia askari hao hata hivyo mtoto huyo aliezaliwa akiwa na miezi nane alifariki muda mfupi baada ya kuzaliwa.
Vyombo vikiwa havina pa kupelekwa
Dogo akiwa ameishiwa Nguvu
 Inasikitisha sana Wanakijiji hawa hawana makazi sasa 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo