PICHA ZA MAZISHI YA MKE WA MASANII WA KUNDI LA WAGOSI WA KAYA DKT JOHN

HUYO hapo katika picha iliyoshikiliwa ndio marehem Bi Estha (37) mke wa msanii Dr John enzi za uhai wake.. Ameacha watoto wanne wa kike katiyao mmoja ana umri wa miezi sita, Bi Estha alifariki baada ya kuanguka ghafla na kukimbizwa hospitali ya kwa mberesero iliyoko Jijini Tanga kwa ajili ya matibabu hapo ndipo umauti ulipomkuta juzi 17/11/2013 Mwili wa marehemu umehifadhiwa nyumbani kwake huko mwakidira Jijini Tanga jana alasiri. R.I.P shemeji.
HUYU ndiye mtoto Irine John aliyeachwa na
umri wa miezi sita..

HAWA ni miongoni mwa wasanii wa kundi la wachekeshaji VITUKO SHOW lilikita kambi huko mkoani Tanga, Kushoto ni Asha Boko na kulia ni Mwene No Disc.

Camera man wa VITUKO SHOW yosso Komando akichomeka mishumaa katika nyumba ya milele ya marehem Bi estha mke wa Dr John.

 
HAPA ndipo alipolala maremu Shemeji yetu M/mungu ailaze mahala pema peponi.

 
MSANII nguli katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya Dr John mwenye T.shirt Nyeusi akiliwazwa na D. dr mwenye T.shirt nyekundu msanii wa Tanga.

DR JOHN akiwa na wasanii na baadhi ya marafiki wakimliwaza baada ya mazishi.
 
PICHA HIZI NI KWA HISANI YA MASAINYOTAMBOFU.COM


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo