MBUNGE
wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa (CCM) Rita Kabati akizungumza na
mwandishi wa habari hizi ofisini kwake mwishoni mwa wiki.(picha na Denis
Mlowe).
======== ====== =======
MBUNGE AVITAKA VYOMBO VYA DOLA KUTENDA HAKI
Na Denis Mlowe,Iringa
MBUNGE
wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa (CCM) Rita Kabati amevitaka vyombo
vya sheria hususan mahakama na Jeshi la Polisi kutenda haki kwa
watuhumiwa wanaofika katika idara hizo wanapopatwa na matatizo na kesi
mbalimbali.
Akizungumza
na mwandishi wa habari Ofisini kwake Kabati alisema hayo baada ya
kutembelea Idara ya Magereza ya Mkoa wa Iringa na kukutana na wafungwa
na mahabusu walimpatia kero zao kwa lengo la kuzifikisha katika mamlaka
husika.
Alisema
watuhumiwa wengi wamevitupia lawama vyombo hivyo kwa kuwasingizia kesi
mbalimbali hususani jeshi la polisi na kwa upande wa mahakama kutoa
vifungo ambavyo wengi wao wamembakiwa na jeshi hilo.
Kabati
alisema mahakama na jeshi la polisi vinatakiwa kufanya uchunguzi wa
kina katika kubaini makosa ya watuhumiwa na kutenda haki kwa kufata
sheria za nchi kuliko ilivyo sasa wengi walioko katika kifungo na
mahabusu wanalalamika kutondewa haki na kubambikiwa kesi ambazo
haziwahusu.
"Mahakama
ni moja ya vyombo vya vinavyotetea haki ya mtuhumiwa hivyo kama mtu
ametenda uhalifu kwa namna yoyote lazima uchunguzi wa kina ufanyike kwa
lengo la kutenda haki kwa watuhumiwa, wengi wao wametoa malalamiko
kuhusu jeshi la polisi na mahakama kuwa rushwa inatawala katika vifungo
vyao na wanaomba msaada wa kusaidiwa kutendewa haki" alisema Kabati
Alisema
viongozi wako kwa ajili ya kutetea haki za msingi za mwananchi na
rasilimali zake na kumletea maendeleo hivyo mahakama na jeshi la polisi
waepuke kuwabambikia kesi wananchi.
Kabati
alisema lazima tuwe wakweli jeshi la polisi limekuwa likielemewa kwa
kiwango kikubwa tuhuma za kuwanyanyasa na kuwakandamiza watuhumiwa
kutokana na malalamiko kutoka kwa wafungwa na mahabusu wenyewe kwa hili
linatakiwa kubadilika.
"Imenisikitisha
sana kwa kuwa kuna watu wanajifanya Miungu mtu katika hizi Idara za
mahakama, na jeshi la polisi kuweza kuwabambikia kesi watu hivyo
kusababisha mrundikano mkubwa wa kesi mahakamani na kujaza watu katika
magereza zetu, mie naomba kabisa wazifatilie na hili jambo sitalifumbua
macho kuanzia sasa na nitalivalia njuga na nitahakikisha kwamba katika
ubunge wangu nilionao hizi changamoto zinatatuliwa kwa wakati" alisema
Kabati.
Alisema
atapigia haki ya wananchi wa Iringa kutoendelea kunyanyasika na vyombo
hivi vya dola kwa kupakaziwa kesi ambazo haziwahusu na kila mwananchi
ana haki ya kutendewa yaliyo mazuri kwa kufuata sheria za nchi.