WALIMU wakuu watatu waliotajwa kuwa ni Margaret Kimbo, Agrey Kikwesha na Lanford Muhando kutoka shule mbalimbali za Tarafa ya Magole wilayani Kilosa, wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali.
Mbali ya vifo vya walimu hao, ajali hiyo iliyotokea baada ya tairi moja ya nyuma kupasuka, imesababisha majeruhi 17, baadhi yao wakiwa katika hali mbaya.
Walioshuhudia walisema kuwa ajali hiyo mbaya ilitokea juzi, majira ya saa 12 jioni katika Kijiji cha Mvumi na Rudewa, eneo la Kisangata mkoani hapo.
Credit: Bongomirror