JACQUELINE WOLPER AZUNGUMZIA SAKATA LA YEYE KUBADILI TENA DINI KWA MARA YA PILI


Hatimaye mwanadada Jacqueline Wolper ameamua kuweka wazi kilichotokea mpaka kuamua kubadili Dini yake ya Uislamu na kurudi kwenye ukristo tena. Kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii mwanadada huyu wa bongo movies ametoa ujumbe ufuatao kwa mashabiki wake.

“…mambo mashabiki zangu.sikua na njia nyingne yakulikwepa hili nanaamini kua kwa wale mashabk zangu waislam amtomaind maana akuna mtu wakumsikiliza chin ya hanga zaidi yawazazi so imenipasa kurudi kanisani kwakauli yawazazi wangu.naamin kama aujaolewa ata uwe na miaka mingap bado unatakiwa kua chin ya imaya ya wazazi ata ukifa ujue unazikwaje na mimi ni binadam sijui saa wala dakika.muhm nikuwajuza nakuwaelewesha mashabik zangu stak maswal nawapenda wote…”

Hapo awali iliripotiwa kuwa mwanadada huyu ameamua kuwa mkristo tena baada ya penzi lake lililosababisha abadili dini na kuwa muislamu na jamaa aitwaye 'Dallas' kuvunjika hivi karibuni.

Swali ni je, atabadili dini tena akitokea mwingine wa dini aliyo tofauti na sasa?


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo