KAYA 30 ZAKOSA MAKAZI BAADA YA MVUA KUBWA KUEZUA NYUMBA ZAO MONDULI

Wananchi wa kaya zaidi ya 30 za kata ya mto wa mbu wilayani Monduli mkoani Arusha hawana makazi baada ya mvua zilizoambatana na upepo mkali kuezua nyumba zao.

Mkuu wa wilaya ya Monduli Bw Jowika Kasunga amesema mvua hizo pia zimesababisha uharibifu  mkubwa katika shule ya sekondari ya Manyara, jengo la hotel na gari moja mali ya shirika la hifadhi za  taifa Tanzania Tanapa ambalo limeangukiwa na ukuta.

Wakizungumzia tukio hilo wananchi walionusurika katika mkasa huo ambao asilimia kubwa  wamehifadhiwa na kwa ndugu na jamaa zao pamoja na kuelezea madhara waliyopata wameiomba  serikali na wasamaria wema kujitolea kuwasaidia.

Akizungumzia uharibifu katika shule ya sekondari ya Manyara mkuu wa shule hiyo amesema wanafunzi  wanne wamepata majeraha madogo na sehemu kubwa ya majengo imeathirika msaada wa haraka  unahitajika.

Eneo hilo wa mto wa mbu ambalo liko kwenye ukanda wa bonde la ufa limekuwa likikubwa na majanga mbalimbali yakiwemo ya upepo mkali na mafuriko jambo linaloonyesha kwamba iko haja ya mamlaka zinazohusika kuchukua tahadhari zaidi hasa ikizingatiwa kuwa idadi ya watu wanaohamia na kuweka  makazi inaongezeka siku hadi siku kwa  mujibu wa  maelezo ya mkuu wa wilaya hakuna mtu aliyepoteza maishakatika tukio hilo
 
CHANZO:ITV


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo