Usaliti! Recho Mathias (23) anadai kumshika ugoni mumewe wa ndoa akiwa na mwanamke ndani ya chumba chake tena kitandani.
Recho Mathias aliyemshika ugoni mumewe.
Habari zilidai kuwa baada ya Recho kukutana na hali hiyo chumbani kwake, moja kwa moja alitoa taarifa kwa viongozi wa serikali ya mtaa ambao walishirikiana na wanaharakati wa jinsia wa FARIJIKA katika ‘kusovu’ ishu hiyo.
Mume wa Recho aliyeshikwa ugoni akiwa na mwanamke.
Ilibainika kuwa kweli ni wanandoa ambapo katika kipindi kifupi cha mwezi mmoja ambacho Recho alikuwa safarini kumuuguza bibi yake, mumewe alichukua mwanamke mwingine kwa makubaliano ya kufunga ndoa.
Mwanamke aliyenaswa na mume wa mtu.
Salha alipoulizwa kama anatambua kuwa mwanaume huyo ana mke alishangaa na kusema kuwa hakuwa akijua chochote zaidi ya kusikia uvumi mtaani.
Recho Mathias (kushoto), kulia ni mwanamke aliyemshika ugoni akiwa na mumewe.
Naye mwanaume huyo alipobanwa na OFM alikataa.
Mwenyekiti wa mtaa (kulia) akiwa eneo la tukio. Kushoto ni mume wa Recho.
Hata hivyo, suala hilo lilipelekwa katika baraza la usuluhishi la serikali za mtaa ambapo Recho na mumewe wanatarajiwa kuitwa leo (Jumatatu) kwa ajili ya kusikiliza shauri lao huku taratibu za kisheria za kushikwa ugoni zikifuatia.
-GPL VIA OFM