ASKOFU WA ANGLICAN DAYOSISI YA NJOMBE AFARIKI DUNIA


Askofu John Simalenga (Pichani) wa Dayosisi ya Njombe Kanisa la Anglikan Amefariki Dunia Asubuhi ya Saa Kumi na Moja Novemba 24 Mwaka Huu na Mazishi Yanatarajiwa Kufanyika Novemba 28 Katika Kanisa Hilo.


Taarifa Toka Kwa Msaidizi wa Askofu Huyo Mchungaji Canon Mlelwa Amesema Kuwa Marehemu Simalenga Amefariki Dunia Baada ya Kuugua Kwa Kipindi Kifupi Kwa Ugonjwa wa Malari na Kisukari Alichogundulika Kuwa Nacho na Hivyo Hadi Kifo Chake Kinamkuta Alikutwa na Malari Mbili.

Aidha Mlelwa Amesema Kuwa Marehemu Askofu Simalenga Amekufa Akiwa na Miaka 60 Ambapo Alizaliwa Mwaka 1953 Katika Kijiji cha Milo Wilayani Ludewa na Uaskofu Alipata Julai 7 Mwaka 2007 Kisha Kuwa Askofu wa 7 Wa kanisa Hilo.
 
Marehemu Askofu Simalenga Ameacha Watoto Wanne na Mjane Mmoja.

Taarifa zaidi Juu ya Msiba Huo Zitaendelea Kukujia Kupitia Mtandao Huu.
 
Na Gabriel Kilamlya


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo