VIJANA WILAYANI MUFINDI WAPATIWA PIKIPIKI 125

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Bi. Jesca Msambatavangu, akifanya uzinduzi wa hafla ya kukabidhi Usafiri wa Pikipiki 125 kwa Chama cha akiba na mikopo, Vijana Sacco's - ya Vijana wa Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa. Bi. Jesca Msambatavangu akitoa ushauri kwa vijana hao, kuacha kubweteka juu ya hatua hiyo ya usafiri wa Pikipiki, ambapo amewataka kuwa na mawazo ya mbele zaidi kwa kujipanga kuwa na magari.
"Pikipiki peke yake hazitoshi, haya chukua na hela hizi shilingi Laki tano zisaidie kuukuza mfuko wa Sacco's yenu vijana, ninawapenda sana vijana wanaojituma, nyinyi kwa mpango huu ni rafiki zangu sana sasa," Alisema Msambatavangu.

 Viongozi wa CCM Wilaya ya Mufindi wakiwa katika hafla ya kukabidhi Pikipiki 125 kwa 'Vijana Sacco's".
 Bw. Felix Lwimbo mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mufindi akiwa na Bw. Edmund Ngalawa katika hafla hiyo ya kukabidhi mkopo wa Pikipiki kwa vijana.
 "Tunasikiliza maelekezo ya viongozi wetu"PICHA NA OLIVER MOTTO
 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo