TANROADS ARUSHA YAFANYA MSAKO WA KUKAGUA MAGARI YANAYOZIDISHA UZITO

Wakala wa bara bara mkoa wa Arusha wamefanya operesheni ya kushitukiza kukagua magari ya mizigo yaliyozidisha uzito na kugundua idadi kubwa ya magari yaliyozidi uzito katika mzani wa mpaka wa Namnga huku baadhi ya magari yakiwa yamezidisha zaidi ya tani thelasini na madereva wake kuyatelekeza na kukimbia kusikojulikana. 

Akizungumza katika operesheni hiyo mkuu wa kitengo cha mizani mkoa wa Arusha Emanuel Mwakyusa amesema operesheni hiyo imefuatia kuongezeka kwa  magari yanayoongeza uzito na kwamba tangu kutolewa kwa agizo la waziri mkuu Mizengo Pinda la kuwataka wamiliki kukaa na serikali kutatua tatizo la ongezeko la tozo za uzito baadhi ya wamiliki wamekuwa wanatumia vibaya nafasi hiyo.

Kwa upande wao baadhi ya madereva wa magari hayo wamesema hali hiyo inasababisha na ubovu wa mizani kwani kila mzani unasoma tofauti huku mizigo ukiwa ni uleule na kuwepo kwa upendeleo wa magari kutoka nje na wengine wakipongeza hatua ya kutoza faini magari yaliyozidisha uzito.

Akizungumzia hali hiyo meneja wa wakala wa barabara mkoa wa Arusha mhandisi Deusidedit Kakoko amesema tuhuma  zinazohusu ubovu wa mizani siyo za kweli bali madereva uongeza mizogo wakiwa njiani na kama kuna wenye uwakika wa tuhuma zake bado kuna nafasi ya kukata rufaa kupinga  adhabu aliyepewa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo