NYOMBO SACCOS YA MKOANI NJOMBE YAWAWAJIBISHA WADAIWA SUGU

 Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba Akiwahutubia Wanachama wa Nyombo Saccos Kijijini Humo.
=======

Na  Gabriel   Kilamlya   Njombe.

Chama cha Ushirika Cha Nyombo Saccos Wilayani Njombe Kimewachukulia Hatua za Kisheria Wanachama wake Nane Katika Kipindi cha Mwaka 2012 Baada ya Kushindwa Kurejesha Kwa Wakati Mikopo Waliyoomba.

Akitolea Taarifa Wakati wa Mkutano Mkuu wa Saccos ya Nyombo Leo Meneja wa Saccos Hiyo Bwana Joseph Mkinye Amesema Kuwa Wanachama Hao Nane Wametaifishiwa Dhamana Zao Kupitia Majembe Auction Mart Ikiwemo Miti na Mali Nyingine Huku Wengine Kesi Ikiendelea Mahakamani.Wanachama Hao Nane Kwa Pamoja Wamebainika Kudaiwa Zaidi ya Shilingi Milioni 11 Hali Iliyopelekea Chama Hicho Kuwachukulia Hatua Za Kisheria Kwa Mujibu wa Kanuni na

Katiba Yao.

Akihutubia Mamia ya Wanachama Wa Saccos Hiyo Kutoka Katika Vijiji Mbalimbali Vya Kata ya Ikuna na Wageni Waalikwa Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba Amewataka Wanachama Kutoogopa Kujitokeza Kukopa na Kwamba Kila Anaye Kopa Ahakikishe Ana Kopa Kwa Malengo Ili Kujikwamua na Umasikini.

Bi.Dumba Pia Amewataka Wanachama Hao Kuona Umuhimu wa Kuongeza Kiwango cha Ununuzi wa Hisa Kwenye Saccos Yao Kwani Hisa Ndio Mtaji wa Chama au Taasisi zozote za Kifedha.

Pamoja na Mambo Mengine Lakini Pia Mkuu wa Wilaya Huyo Amesema Serikali Inaendelea Kutoa Ushirikiano Mkubwa Kwenye Vyama Mbalimbali vya Ushirika Kwani Vyama Hivyo Vimeonekana Kuwasaidia Sana Wananchi Wenye Hali ya Chini Kiuchumi.

Chama cha Ushirika Cha Akiba na Mikopo Nyombo Saccos Kilisajiriwa Mnamo Mwaka 1999 Februari 11 Ambapo Katika Kipindi cha Mwaka 2012 Kimefanikiwa kupata Faida ya Zaidi ya Shilingi Milioni 11 Ambazo Mkutano Huo Mkuu wa Mwaka Uliofanyika Oktoba 26 Umeridhia Faida Hiyo Kugawana Kwa Wanachama Wote.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo