
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini
(TASWA),Juma Pinto akizungumza na Waandishi wa Habari jioni hii nje ya
Ukumbi wa Mikutano wa Water Front,kunakofanyika Uchaguzi wa Rais na
viongozi mbali mbali wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) ambapo hadi sasa
hakuna Mwandishi yeyote alieruhusiwa kuingia kwenye Ukumbi huo kwa
madai kwamba Waandishi hawausiki na Uchaguzi huo,kwani waandishi jukumu
lao ni kusubiria kupewa matokeo tu ya uchaguzi huo,kauli iliyotolea na
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi,Ndg. Hamidu Mbwezeleni.Jambo hilo
liezua tafrani kidogo kwenye Eneo hilo hasa pale Watu wa Usalama
(Polisi) walipowataka Waandishi kuondoka kwenye Eneo hilo la
Uchaguzi.Mwenyekiti wa TASWA,Juma Pinto amewataka Waandishi wa Habari
kuachana na Uchaguzi huo na kutoripoti chochote,kwani kilichoonyeshwa ni
dharau kubwa kwa waandishi wa Habari na watanzania wote nchini
wanaopenda Michezo.