Mstahiki
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akikabidhi
rasmi Magodoro 50 kwa Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini
Dar.
Mstahiki
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akimshukuru
Mwenyekiti wa kikundi cha Neema Womans Power Bi.Maryam Dedes (mwenye
hijabu nyekundu) mara baada ya kukabidhi Magodoro hayo.
Mwenyekiti
wa kikundi cha Neema Womans Power Bi.Maryam Dedes katika picha ya
pamoja na Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na Wakinamama
wa Kikundi cha Neema Womans Power.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akiwa ameongozana na
Mwenyekiti wa kikundi cha Neema Womans Power Bi.Maryam Dedes kuelekea
kwenye chumba cha mikutano katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kabla ya
kukabidhi msaada wa Magodoro kwenye Hospitali hiyo.
Mkurugenzi
wa Wauguzi Hospitali ya Muhimbili Bi. Agnes Jonathan Mtawa akizungumzia
changamoto mbalimbali zinazowakabili katika uotaji huduma kwa wananchi
mbele ya mgeni rasmi Mstahihiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa
katika hafla fupi ya kukabidhi Magodoro 50 kwa Hospitali hiyo.
Katibu wa Neema Womans Power Mgeni Ottow akisoma risala yao mbele ya mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akizungumza kwenye hafla fupi
ya kukabidhi Magodoro 50 kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Na. Ripota wetu.
Mstahiki
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala MH.JERRY SILAA amekabidhi
magodoro 50 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupitia kikundi cha
wakimama "NEEMA WOMANS POWER".
Neema
Womens Power ni kikundi cha wakina mama kilichoanzishwa mwaka 2005 kwa
kuanza na Madrasa mbili ya akinamama na wasichana akiwa na wanafunzi 18
tu. Madrasa hizo zipo Kinondoni na Buguruni chini ya Mwenyekiti wa
kikundi hicho Bi.Maryam Dedes. Jumuiya hii pamoja na kuwa na Elimu ya
dini, husaidia jamii kwa michango mbalimbali ikiwemo kulipia ada za
shule kwa wanafunzi wasiokuwa na uwezo, kusaidia Walemavu na Wajane
pamoja na familia duni.
Katika
hafla hiyo fupi Mgeni rasmi Mh. Jerry Silaa ametoa wito kwa wadau
mbalimbali kuweza kujitoa kwa kusaidia jamii kwani mzigo uliopo kwa
Serikali peke yake haiwezi, na ukizingatia ya kwamba hakuna mtu
asiyeijua Hospitali kama si Muhimbili basi Amana, Temeke au
Mwananyamala na Hospitali nyingine nyingi zinahitaji msaada vifaa
mbalimbali na endapo kila mwananchi angeweza kuchangia japo kifaa
kimoja sasa tungekuwa mbali sana na inawezekana kabisa tusingekuwa na
matatizo sugu katika Hospitali zetu.
Mh.Jerry
ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha huduma zinaboreshwa
ndani ya Halmashauri yake na anayesifika kwa uchapakazi wake na umakini
aliwashukuru kwa dhati kabisa uongozi wa Neema Womans Power pamoja na
wanachama wao kwa kuliona tatizo hilo na kwa uwezo walionao leo hii
wameweza kutoa magodoro hayo 50 na kuwaasa waendelee kujitoa zaidi na
wasife moyo maana kazi ya jamii haina malipo zaidi ya fadhira mbele za
Mungu.
Hafla
hiyo fupi ya kukabidhi Magodoro imehudhuriwa na Bi.Maryam Dedes ambaye
ni Mwenyekiti wa kikundi hicho, Agnes Jonathan Mtawa- Mkurugenzi wa
Wauguzi Hospitali ya Muhimbili, Mgeni Ottow Katibu wa Neema Womans Power
pamoja na Khadija Mwita Makamu mwenyekiti na wajumbe wao 30 na Uongozi
wa Hospitali ya muhimbili.