JUKWAA LA KATIBA LAIPASHA TUME YA KATIBA MPYA

 Mwenyekiti  wa  jukwaa la katiba nchini Tanzania Bw  Deusi  Kibanda akitoa  mada  katika  tamasha la 11 la  mtandao  wa  jinsia Tanzania (TGNP )  leo   katika viwanja  vya  TGNP Mabibo  jijini  Dar es Salaam

 Bw Kibanda akisisitiza jambo katika  tamasha  hilo la TGNP  leo
 Baadhi ya  washiriki wa  tamasha hilo  wakifuatilia  hotuba ya  Bw  Kibanda  leo
 Mwenyekiti  wa  jukwaa la katiba  Bw  Deusi Kibanda akitafsili lugha  ,wakati  mshiriki  wa tamasha la TGNP kutoka  nchini Uganda wakati  akichangia  kuhusu rasimu  ya  katiba  ya  Tanzania
WAKATI  mchakato  wa  rasimu ya  katiba  ukiendelea  ,mwenyekiti  wa  jukwaa la katiba Deusi Kibanda  amewataka  wanawake  nchini kutokubali  kuipigia  kura rasimu  ya  katiba  mpya  iwapo maoni  mbali  mbali  yaliyotolewa na  wanawake hasa  masuala  ya  usawa  wa  kijinsia  yasipoingizwa  katika  rasimu  hiyo.
Akitoa mada  juu ya  mchakato  wa katiba  ya Tanzania kwenye  tamasha la 11 la mtandao  wa  kijinsia  Tanzania  (TGNP) leo  ,Kibanda  amesema  kuwa asilimia  zaidi ya 70  wapiga  kura nchini ni  wanawake  hivyo maoni  ya  wanawake  kama hayatasikilizwa na  kuwekwa mambo  ambayo hayamtetei  mwanamke  na motto  katika  rasimu  hiyo ya katiba  basi  wanawake  nchini  wasikubali  kuipigia  kura .

Kwani  alisema  mbali ya  tume  hiyo ya katiba  kuwa na  wanawake ndani yake  ila bado kwa  sehemu  kubwa  wameonyesha  kushindwa  kupigania maoni  ya  wanawake  kuingia  katika rasimu  hiyo ya katiba.
Kibanda  alisema  kuwa  wakati  mchakato  huo  ukielekea  kufika  mwisho  kwa  kuwa katika  hatua  ya mabaraza la  katiba kupitia  rasimu  hiyo  ya katiba  ila  yamekuwepo  mapungufu  mbali mbali  katika rasimu  hiyo  baada ya  maoni mbali mbali  yaliyotolewa na  wanawake  kutoingizwa  katika rasimu  hiyo.

Hivyo alisema  kama  tume ya katiba  itaendelea  na msimamo  wake  wa  kutoingiza maoni sahihi  ya  wananchi  katika rasimu  hiyo  watambue  kuwa  hatua ya  mwisho  baada ya  bunge  la katiba  ni wananchi  kuipigia kura katiba  hiyo  jambo ambalo wananchi wanapaswa kuwa makini na kama  itakuwa kimya  bila  kuingiza masuala  ya usawa wa kijinsia .  

Bw Kibanda  alisema  kuwa katiba  nzuri  ni ile ambayo  itayatazama makundi  yote  katika  hali ya  usawa  wa asilimia 50 kwa 50 vinginevyo katiba  haitakuwa na maana  kama  itakumbatia  mfumo  dume  na rasilimali za nchi  zikawanufaisha   wachache .

“ Mchakato  huu  wa  rasimu  ya katiba  unaendelea  ila bado ukitazama  vema  unaona bado katiba imempa mamlaka  makubwa zaidi Rais ya  kuteua badala ya  kupeleka mamlaka  hayo kwa  bunge ambalo ni sauti  ya  wananchi”

Wakati  huo  huo Katibu wa jumuia ya Wanawake na watoto( SHIVYAWATA) Rebecca Eliazar ameeleza changamoto  zinazowakabili  watu  wenye  ulemavu Eliazar alisema kuwa  ukatili kwa wanawake walemavu umekuwa mara mbili ya ule wanaofanyiwa watu wa anina nyingine kwani wamekuwa wakidharauliwa huku wakionwa kuwa wao hawana hata haki ya kueza kuzaa na kua na familia.

”Watu wamekua na tabia kuona kuwa ukifanya tendo la ndoa na Mlemavu wa kike unaweza kutoa nuksi au kupata utajiri wa haraka na kuheshimiwa katika jamii”, Alisema Rebecca Eliazar katika warsha hiyo.


Pamoja na mambo mengine katika Warsha hiyo  Eliazar aliendelea kusema kuwa huduma mbovu wanazopatiwa walemavu katika vituo vya Afya si rafiki na watu wa jamii hiyo hasa katika suala zima la vitanda kuwa juu na hivyo kupata shida kupanda.


Alindelea kusema kuwa Lugha chafu za dharau kwao pamoja na matusi pia vimekuwea mstari wa mbele wa watu hao hali ambayo inawapa wasiwasi hata wanapopata matatizo ya kuugua,.


Hata hivo Eliazar alisema kuwa watu wakikuona Mlemavu umepata ujauzito wanakutolea lugha mbaya ikiwa ni pamoja na dharau kna kwamba mlemavu wa kike hana haki ya kupata mtoto au kumiliki familia.


“Ukiwa mjamzito ukipishana na watu utasikia watu wanasema kuwa kuwa,


Mwangalieni huyu hajioni hali yake halafu anabeba ujauzito kwanza aliyekupa mimba mimba ni nani?”, Aliongeza Rebecca Eliazar.


Kwa upande wake Mwezeshaji kutoka katika Shirika la Plan Internation


Anna Mushi alisema kuwa mfumo wa kutopata Elimu ya afya ya uzazi kwa watoto ndio chanzo kikubwa cha mimba za utotoni.

Pia Mushi katika Warsha hiyo aliataka wanawake kuwa na amri juu ya miili yao hasa katika suala zima la uzazi hali ambayo itapunguza umasikini katika familia zao na kuchangia haraka shughuli za maendeleo.

Mkurungezi  wa TGNP  Usu Mallya  alisema  kuwa  baada  ya  hitimisho  la tamasha  hilo la 11 washiriki  wote  zaidi ya  2000  wanaoshiriki  tamasha  hilo kwa mwaka  huu  kutoka mikoa mbali mbali  Tanzania  bara na visiwani  watasaini tamko maalum ambalo litaandaliwa na washiriki  wa tamasha  hilo  kuhusu mchakato  wa katiba na tamko  hilo litafikishwa  katika  bunge la katiba kama mapendekezo  ya  wanawake nchini  juu ya rasimu  hiyo ya katiba.
 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo