Habari nilizopata hivi punde kutoka vyanzo vya kuaminika
ni kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon kupitia kwa Mshauri
wa UN katika ukanda wa Maziwa Makuu, Bi Mary ROBINSON, amemshauri Rais
wa Tanzania JAKAYA KIKWETE kuhudhuria mkutano wa ICGLR unaofanyika
Jijini Kampala, Uganda. Sababu zilizotolewa ni kama ifuatavyo
- Mkutano huo umepewa baraka zote za UN na kwamba umoja huo umetuma mwakilishi kuhudhuria kikao hicho ambaye ni Bi Mary Robinson
- Mkutano huo utajikita katika
kujadili jambo moja tu ambalo ni hali ya amani mashariki mwa DRC na
hautahusisha mazungumzo baina ya JK na PK kutokana na kupishana kauli
katika siku za hivi karibuni.
- Kutokana na Tanzania kupeleka
kikosi kupambana na waasi wa M23, Tanzania itapewa nafasi ya kuelezea
mafanikio yaliyopatikana kutokana na operesheni hiyo na kwamba nchi zote
za maziwa makuu zitatakiwa kuunga mkono juhudi za Tanzania
- Nchi washiriki watapewa makavu
na Bi Mary Robinson kutokana na nchi hizo kuwa na tabia ya kuchochea
migogoro DRC. Hapa walengwa wakubwa ni Rwanda na Uganda. itakumbukwa
kuwa hivi karibuni Katibu Mkuu wa UN Ban Ki Moon amemshutumu Rais wa
Rwanda PK kutokana na kusaidia waasi wa M23. Pia Afrika ya Kati
inashutumiwa kusaidia waasi wa LRA.
- Usalama wa viongozi wote watakaohudhuria kikao hicho umeimarishwa na utakuwa ni jukumu la UN
- Tanzania kama nchi mama ya
Maziwa Makuu, ni vema kuhudhuria mkutano huo kwa vile usalama wa nchi
jirani unapozorota, ni Tanzania ndiyo inayoathirika hasa kupitia wimbi
la wakimbizi, wahamiaji haramu na kuzagaa kwa silaha za kivita.
Kutokana na Mazungumzo hayo ambayo yamefanyika kwa njia ya simu baina
ya Rais JK na Bi Mary Robinson, Rais JK amelazimika kusitisha ziara yake
Mkoani Mwanza na kupanda ndege kuelekea Kampala Uganda jana jioni
(tarehe 4/5/2013). Hivi tunavyozungumza Rais wetu amewasili salama na
anahudhuria mkutano huo. Aidha, inaelezwa kuwa Rais wa Rwanda Paul
Kagame mpaka leo asubuhi alikuwa hajathibitisha kuhudhuria na huenda
asihudhurie kikao hicho ili kukwepa kibano cha Mwanamama Mary Robinson
CHANZO: JAMII FORUM
