MKUTANO WA CHADEMA UKONGA JIJINI DAR

Kama ilivyotangazwa awali CHADEMA leo wamefanya mkutano mkubwa wa hadhara katika jimbo la Ukonga Eneo la Mazizini. 
 
Mkutano huo ulihutubiwa na Mwenyekiti wa Bavicha Taifa John Heche akishirikiana na vijana wa Bavicha Jimbo na viongozi wa Jimbo na Kata.

Yaliyojiri mkutanoni:

Mkutano huu ulikuwa ni wa Kata tu lakini cha kustaajabisha ulihudhuriwa na umati mkubwa wa watu kiasi kwamba ulionekana ni mkutano wenye hadhi ya kitaifa.Mjumbe wa Sekretariati ya Bavicha Taifa aliyeongozana na Heche alisema vijana wameamua kuleta mageuzi na watapambana bila kuogopa chochote alimradi wanafuata sheria na taratibu.
 
Katibu wa Jimbo la Ukonga Sheikh Mwaipopo akihutubia umati mkubwa wa watu alilaani CCM kwa kuendesha propaganda za udini na sasa zinahatarisha amani ya nchi.
 
Huku akishangiliwa na halaiki ya watu Sheikh Mwaipopo amesema Waislam wamegundua propaganda za CCM na kwa kuthibitisha hilo amesema jana aligawa kadi kwa Masheikh 12 wa Gongolamboto walioomba kwa hiyari yao kujiunga Chadema.
 
Akizungumza katika mkutano huo mgeni rasmi Mkiti wa Bavicha Taifa John Heche alilaani CCM kwa kukataa mapendekezo yote ya msingi yaliyoko katika Rasimu ya Katiba mpya.
 
Heche amewaambia wananchi kwamba kuanzia kesho Chadema inaanza ziara katika nchi nzima kutumia anga na nchi kavu kuelezea msimamo wa Chadema kuhusu katiba mpya.
 
Katika hali ya kusikitisha wananchi walihuzunika sana baada ya Heche kuwaeleza jinsi wabunge wa CCM walivyovizia kipindi ambacho Chadema hawakuwepo bungeni na kupitisha harakaharaka kodi ya laini za simu.
 
Mara baada ya mkutano huo wananchi waligawiwa bure Nakala za rasimu ya katiba bure.Kwa muda mchache nakala zaidi ya mia mbili ziliisha na pia mamia ya wanachama wapya walichukua kadi za Chadema na mpaka naandaa taarifa hii bado kulikuwa na foleni kubwa ya wanachama wanaosubiri kadi mpya.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo