Gari hili linalodhaniwa kuwa la Serikali nalo lilihusika kubeba abiria
Moja kati ya Magari yakingoja kubeba Abiria katika kituo cha Mwanjelwa
Noah nazo hazikuwa nyuma
Moja ya Gari ambalo lilikuwa likingoja kuchukua Abiria
Askari wa usalama wa Barabarani akisimamia usalama wa Magari na Abiria
Abiria wakiwa tayari kwa safari kuelekea wilayani
Safari ndio hiyooo........... inaendelea
Moja kati ya Magari ambalo nalo lilikuwa likingojea kubeba Abiria
Gari hii kubwa aina ya Fuso nalo Lilikuwa linatoza nauli kwa Tsh 4000 mpaka Tukuyu
Makubwa haya... Hata Gari za nje ya Nchi nazo zilikuwa zikifanya Biashara
Hawa Abiria wote wapo tayari kuwachukua Abiria.....
Ezekiel Kamanga
Shughuli za kiuchumi kwa Wakazi
wa Mkoa wa Mbeya Leo zilisimama kwa siku nzima hususani kwa wasafiri
wanaotumia usafiri wa mabasi aina ya Coaster baada ya madereva ma mabasi hayo
kugoma.
Kutokana na hali hiyo ya mgomo huo
shughuli za kiuchumi zilidorora kwa kiasi kikubwa na baadhi yao kushindwa kwenda kazini baada ya
madereva na wamiliki wa vyombo hivyo kushindwa kutokea barabarani na kuleta
adha kubwa.
Hata hivyo ililazimu kupatikana
njia ya dharua ambapo maroli yalilazimika kutoa huduma ya usafirishaji wa
abiria na mizigo kwenda Wilaya za Kyela,Mbozi,Rungwe na Tunduma wilaya ya
Momba.
Hali hiyo ilipelekea kamati ya
ulinzi na usalama ya mkoa kukutana kwa dharula ili kupata mustakabali wa suala
hilo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa pamoja na Umoja wa Madereva wakiongozwa na
chama cha wasafirishaji.
Madereva hao walimshukia lawama
Meneja wa SUMATRA Mkoa kuwa ndiye chanzo kwa kuwatoza faini kubwa na wakati
mwingine fedha wanazolipa kutopatiwa stakabadhi hali inayotia shaka.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama
cha wafanyakazi wasafirishaji Bwana Ezekiel Mwakapala amesema kuwa wao
hawajagoma bali wameona ni afadhali kutotoa magari barabarani kuliko kutoa pesa
nyingi kwa SUMATRA.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi
Mkoani Mbeya Diwani Athuman amesema hajafurahishwa na kitendo hicho kwani
migogoro inatatuliwa kwa njia ya mazungumzo na kitendo cha kugoma kinawaumiza
wananchi wasio na hatia.
Kamati ya ulinzi na usalama
iliuagiza uongozi wa wasfirishaji abiria kuleta malalamiko yao ili yaweze
kushughulikiwa na kupata ufumbuzi wa kudumu.
Baadhi ya wenye maroli walifurahia
huduma hiyo wakidai kuwa magari yao yalikuwa yakiegeshwa bila bila kazi kutwa
nzima na kwamba nauli zilikuwa zikitozwa kati ya shilingi elfu tatu hadi elfu
kumi kutoka Mbeya kwenda Kyela au Mbeya kwenda Tunduma na Jeshi la Polisi
liliimarisha usalama barabarani kuhakikisha wasfiri hawapati bughudha yoyote
njiani.
Baada ya kikao kutoka ofisi ya Mkuu
wa Mkoa madereva na wamiliki wa vyommbo hivyo walikuwa wakikutana katika ofisi
zao zilizopo ofisi za nane nane.