DK MAHANGA NA WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU WAKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA MIUNDOMBINU SEGEREA

 Mbunge wa Jimbo la Segerea, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akiwaonesha wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ilala (Jimbo la Segerea), kituo kipya cha Polisi cha Tabata, Dar es Salaam, walipokuwa kwenye ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu jimboni humo.
 Dk. Makongoro Mahanga na Diwani wa Kata ya Tabata, Mtumwa Mohamed pamoja na wajumbe wakikagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa manne akatika Shule ya Msingi Tabata
 Dk. Mahanga akitoa maagizo kwa watendaji wa Kata ya Kimanga, kuhakikisha wanabomoa haraka msingi wa bendera ya CHADEMA, uliojengwa kwenye eneo la Stendi ya Dcaladala ya Kimanga inayotarajiwa kufanyiwa matengenezo wiki hii.
 Dk. Mahanga akizungumza wakati wa kukagua ujenzi wa daraja la maji ya chumvi.
 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Ilala, wakikagua maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kinyerezi- Segerea.
 Mhandisi wa Manispaa ya Ilala, Muhinda Kassim akitoa ufafanuzi kuhusu maendeleo ya ujenzi wa miradi
 Mkazi wa Kinyerezi akitoa ushauri kwa wahandisi wa Tanroads Dcar es Salaam kuhakikisha wanatunza vizuri barabara ikiwemo kuwela alama.
 Mmoja wa wahandisi wa Tanroads akielezea kuhusu maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kinyerezi-Segerea
 Wajumbe wakiwa site ya daraja hilo
 Dk. Mahanga akizungumza na wahandisi wa Tanroad Mkoa wa Dar es Salaam
 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ilala, wakikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Tabata-Liwiti.
 Mhandisi Mwandamizi wa Tanroads DSM, Eliakim Tenga akielezea kuhusu maendeleo ya ya ujenzi wa barabara ya Tabata-Liwiti.
Msafara wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ilala, ukiwa kwenye magari ukikagua maendeleo ya ujenzi wa Barabara ya Liwiti-Baracuda.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo