Waombolezaji
wakimsikiliza mchungaji wa KKKT aliyendesha ibada fupi ya kumuaga
marehemu huyo iliyofanyika katika kanisa lililopo Hospitali ya Taifa
Muhimbili.
Ndugu wakiwa wamekaa kwa simanzi kanisani hapo.
Mchungaji akiaga mwili wa marehemu.
Waombolezaji wakitoka nje ya kanisa kwa huzuni baada ya kumuaga mpendwa wao.
KUFUATIA kukithiri kwa matukio ya ujambazi
jijini Dar Salaam, mfanyabiashara mwingine (jina linahifadhiwa kwa
sababu maalum) amepigwa risasi na kufa papo hapo. Tukio hilo lilitokea
Temeke.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke,
Albert Kiondo, majambazi hayo yalimtwanga risasi mfanyabiashara huyo na
kutoweka yakiwa na pikipiki bila kuchukua kitu chochote.
Yafuatayo
ni matukio yanayohusu kuagwa kwa mwili wa marehemu huyo aliyesafirishwa
kupelekwa kwao mkoani Kilimanjaro leo kwa ajili ya mazishi. (Picha habari/ Haruni Sanchawa / GPL)
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi