Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts (kushoto) pamoja na wenzake wakimpa pole Nizar Khalfan (kulia mwenye kofia). Nizar (kushoto) akisalimiana na Said Bahanuzi.…Haruna Niyonzima akimpa pole Nizar. Pembeni ni Jerry Tegete.Baadhi ya wachezaji wa Yanga wakiwa msibani.Nizar akiongea na kocha wake pamoja na alioambatana nao.Brandts akimuaga Nizar.
KOCHA
Mkuu wa Yanga Ernie Brandts leo amekiongoza kikosi chake kufika
nyumbani kwa kiungo wake Nizar Khalfan ambaye alifiwa na baba yake mzazi
juzi jioni.
Nizar
alifiwa na mzazi wake huyo aliyejulikana kwa jina la Khalfan Khalfan
Jumamosi iliyopita baada ya kuugua kwa muda mfupi na kulazwa katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimmbili ambako umauti ulimkuta.
Mara
baada ya kutua nyumbani kwa Nizar kikosi hicho kikiwa na nyota
mbalimbali walitoa mkono wa pole kwa Nizar pamoja na mdogo wake Razak
Khalfan ambaye ni kiungo wa Coastal Union ya Tanga.
PICHA KWA HISANI YA GPL