Miili ya Askari wa Jeshi la Wananchi wa
Tanzania JWTZ waliouawa Darfur wiki iliyopita Sajent Shaibu Shehe
Othuman wa Mpendae na Koplo Mohamed Juma Ali wa Kwarara imekabidhiwa leo
kwa familia zao mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Zanzibar.
Marehemu hao wawili wenye Asili ya
Zanzibar ni miongoni mwa Askari saba wa JWTZ waliuawa walipokuwa
wakilinda amani chini ya Umoja wa Mataifa na Afrika UNAMID,huko Darfur.
Miili ya marehemu hao imewasili majira ya
saa 9 alasiri kwa ndege ya JW 90 34 aina ya Boing ikitokea katika
Hospitali ya JWTZ Lugalo Jijini Dar es Salaam.
Mara baada ya kuwasili Uwanjani hapo
Miili ya Marehem hao ilipokelewa na Katibu mkuu Afisi ya Makamu wa Pili
wa Rais Khalid Mohamed Salum akifuatana na Mwenyeji wake Bregedia
Jeneral Kamanda wa Bregedi ya Nyuki Sharif Sheikh Othuman Viongozi wa
Vyama na Serikali,Wanafamilia pamoja na Wananchi kwa ujumla.
Aidha huzuni ziliendelea kutanda kwa
ndugu na Jamaa waliofika kupokea maiti hizo za Wapiganaji wa Amani ya
Dunia chini ya mwenvuli wa UNAMID.
Kwa mujibu wa Taarifa kutoka Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais Shughuli za Mazishi zitafanyika kesho saa nne za
asubuhi katika makaburi ya Mwanakwerekwe nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Aidha shughuli hiyo ya Mazishi itaambatana na taratibu za kijeshi zitakazofanyika Makaburini hapo.