Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi
akizungumza katika Mkutano wa Teknolojia ya Kupambana na Uhalifu uliofanyika
katika Jiji la Lyon nchini Ufaransa hivi karibuni. Waziri Nchimbi alishiriki
mkutano huo pamoja na washiriki wengine kutoka nchi mbalimbali duniani.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (katikati) akimsikiliza kwa makini Rais wa Shirika la Kimataifa la Polisi (Interpol), Mireille
Ballestrazzi (kushoto) baada ya Mkutano wa Kimataifa wa Teknolojia ya
Kupambana na Uhalifu uliofanyika katika Jiji la Lyon nchini Ufaransa
hivi karibuni. Kulia ni Meya wa jiji hilo, Gerald Collomb.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na
Rais wa Shirika la Kimataifa la Polisi (Interpol) Mireille Ballestrazzi
(kushoto) na Kulia ni Meya wa Jiji la Lyon, Gerald Collomb. Waziri Nchimbi
alishiriki mkutano huo wa Kimataifa hivi karibuni.
PICHA ZOTE
NA
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.