
Timu
ya wekundu wa msimbazi ya simba sport club ya jijini Dar es salaam
imezuru kaburi la baba wa taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere na
kutangaza kuwa baraka walizozipata zitawawezesha kunyakuwa ubingwa wa
ligi kuu ambayo inatarajiwa kuanza hivi karibuni.
Timu
hiyo ikiongozwa na kocha mkuu wake Abdallah Kibadeni na msaidizi wake
Jamhuri Kihwelo,baada ya kuwasili katika eneo la Mwitongo imepokelewa na
mjane wa baba wa Taifa Mama Maria Nyerere,kisha kudhuru katika kaburi
la mwasisi huyo wa taifa la Tanzania na kuweka mashada ya maua katika
kaburi hilo