AGONGA KILABU CHA POMBE NA KUJERUHI KADHAA WAKATI AKIJIFUNZA KUENDESHA GARI TANGA

 
Watu wanne wamejeruhiwa mmoja wapo vibaya sana kufuatia dereva aliyekuwa akijifunza kuendesha gari kwenda kuparamia watu waliokuwa katika baa ya pombe za kienyeji  inayojulikana kwa jina la Ukumi iliyopo katika eneo la Usagara jijini Tanga.
 
Waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni mzee Ally Kangajaka mwenye umri wa miaka 68,Juma Sabas Baharia wa mamlaka ya bandari Tanga, Millian Mngazija mama lishe na Godfrey Msagati ambaye amejeruhiwa vibaya sehemu za kichwani ambapo wote wamelazwa katika hospitali ya rufaa mkoani Tanga wanaendelea na matibabu.

Wakielezea tukio baadhi ya mashuhuda wamesema dereva aliyejulikana kwa jina la Juma Mwinzari alichukua gari la mmiliki anayejulikana kwa jina la Mussa Shemkhai na kuliendesha ndipo lilipomzidi nguvu na kwenda kuparamia watu waliokuwa katika kilabu cha pombe za kienyeji cha Ukumi kisha kugonga ukuta. 

Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa katika eneo la tukio wamedai kuwa baada ya ajali hiyo mmiliki wa gari alikuwa akijiandaa kuliondosha gari hilo kabla askari hawajafika ndipo alipokutana na baadi ya vijana waliotaka kumpiga wakimtaka aliache gari hilo hadi askari watakapopima kwa mujibu wa sharia. 
 
Kufuatia tukio hilo jeshi la polisi linawashikilia watu wawili, mmiliki wa gari hilo na mtuhumiwa ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
 
ITV


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo