SIKU YA MASHUJAA MWAKA HUU KUFANYIKA MKOANI KAGERA

JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA                 11 Julai, 2013

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linaadhimisha siku ya mashujaa kila tarehe 25 Julai, ikiwa ni sehemu ya kuwakumbuka mashujaa waliopigana na kushinda vita ya Kagera mwaka 1978/1979.

Maadhimisho hayo  hufanyika mara moja kwa mwaka, na mwaka huu yatafanyika tarehe 25 Julai 2013 katika mkoa wa Kagera wilaya ya Bukoba kwenye makaburi ya mashujaa yaliyopo Kaboya.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo atakuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. JAKAYA MRISHO KIKWETE.

Sambamba na mgeni rasmi, watakuwepo viongozi waandamizi wa Serikali, vyombo vya Ulinzi na Usalama, vyama vya siasa, taasisi za dini na taasisi mbalimbali za kiraia.

Vyombo vya habari vinaalikwa kushiriki katika maadhimisho hayo ambayo ni muhimu kwa Taifa.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP 9203, Simu: 0764742161

Email: ulinzimagazine@yahoo.co.uk


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo