Baadhi ya askari polisi wakionyesha kwa waandishi wa habari silaha zilizokamatwa kutoka kwa watuhumiwa wa matukio ya ujambazi.
DCP
Mlege akitoa taarifa ya mafanikio ya Jeshi hilo kwa waandishi wa habari
ambapo akizungumzia suala la Mh. Mnyika amesema askari No. E. 5340
D/CPL Julius aliyekuwa ndani ya gari la polisi PT. 1902 alikuwa
anasogeza boksi lenye mabomu ya kutoa machozi ya kurusha kwa mkono, kwa
bahati mbaya bomu hilo lililipuka ndani ya gari hilo na halikuleta
madhara yeyote kwa askari polisi wala raia waliokuwa eneo la uwanja wa
Sahara uliopo Mabibo ambako chama cha CHADEMA kilikuwa kifanye mkutano
wa hadhara tarehe 21 Jula 2013 kinyume na utaratibu.
Jeshi
la Polisi Kanda maalum Dar es Salaam limefanikiwa kukamata sila 5
ikiwemo SMG moja, Shortgun mbili, Riffle Mark 3 tatu, Pisto moja, Risasi
56, Maganda ya Risasi 17 na Majambazi 8.
Akizungumza
na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Kamishna wa
polisi kanda hiyo, DCP A.M. Mlege amesema zoezi hilo lilifanyika Julai
18 mwaka huu katika maeneo ya Magomeni wilaya ya Kinondoni.
Amesema
pia Jeshi hilo limeweza kukamata magari ya wizi matano, Injini tatu za
magari, Vipande vya magari yaliyokatwa spea na wezi watano wa magari.
Katika
hatua nyingine Jeshilo limekanusha habari zilizotolewa katika vyombo
vya habari kuwa mbunge wa Jimbo la Ubungo Mh. John Mnyika kukoswa na
bomu na kumjeruhi mmoja wa wafuasi wake.
Aidha limeomba siku zingine kabla ya kutoa habari ni vizuri likaulizwa ili kuthibitisha au kukanusha.
DCO
Mlege amesema pia Jeshi la polisi Kanda maalum Dar es Salaam
limemkamata tapeli hatari anayetumia namba tofauti za mitandao ya simu
na majina ya watu maarufu anajulikana kwa jina la Mfaume Omari maarufu
kama ‘Mau’.
CREDITS:MO BLOG