Wema Sepetu Ceo wa Endless fame films Swahiliwood.
HIVI sasa kuna vita inayofukuta chini kwa chini kati ya watayarishaji
wakubwa kutoka kundi kubwa la Bongo Movie linaloitwa Big Five, vita
hiyo ambayo watafiti wa mambo bado hawajaelewa sababu inayoleta uhasama
kati ya watayarishaji hao na mwanadada huyo mwenye makeke mjini, kundi
hilo limepanga kumpoteza kabisa Wema katika tasnia ya filamu.
Wema akiwa katika pozi
Moja ya sababu kubwa ambayo imezua ugomvi huo ambao pengine hawataki
kabisa ujulikane ni sababu ya Wema kufungua kampuni yake ya uzalishaji
wa filamu ya Endless fame film ambayo pengine imeonekana kuja kisasa
zaidi na kuweza kutoa ajira hata kabla ya kuwa na kazi nyingi za kufanya
za filamu.
.
Wema Sepetu akiwa moja ya picha
“Pengine watu wanaweza kutafsiri vibaya si Wema pekee yake tu ambaye
amekuwa ni tatizo kubwa katika tasnia ya filamu, hawa dada zetu bwana
wanatuangusha sana kwani wao wakiandaa filamu zao hawatumii pesa za
mitaji yao, wanawezeshwa na jamaa zao, lakini wakifika sokoni kwa sababu
hawana uchungu nazo wanauza bei ya kutupa,”anadai mdau huyo.
Awali ilikuwa ni kama utani ambao kila aliyesikia hakujua kama
inaweza kufikia hapo ilipo sasa, Wema mwenyewe haoni kama ni tatizo kuwa
na kampuni ya Production na kuzalisha kazi zake, lakini mwenyewe anaona
ni moja kati ya kuongeza ajira wala haoni kama ni mshindani.
Mwenyewe anahisi pengine kuwa na msimamo inaweza ikawa ni njia
mojawapo ya kumjengea maadui, kwani mara nyingi watayarishaji wengi
wanawapangia waigizaji fedha ya kuwalipa na si waigizaji
Na FC