Hiyo ndiyo Baiskeli iliyokuwa ikitumiwa na Marehemu kabla ya Mauti Kumkuta.
Hii ndio Pikipiki iliyosababisha Ajali Mbaya Leo ya Mwendesha Baiskeli na Kusababisha Kifo Papo hapo.
Hii ndio
Barabara inayotumiwa kwa Kasi Kubwa baada ya Kulimwa na Hivyo
Kusababisha Ajali za Mara kwa Mara Wilayani Wanging'ombe.
Mwili wa Marehemu Linus Nziku mkazi wa Mdasi Wanging'ombe ukiwa Umefunikwa na Kuondolewa Katikati ya
Barabara alipogongwa.
Barabara alipogongwa.
Mwendesha
Baiskeli Marehemu Linus Nziku[45] aliyegongwa na Kufariki Papo hapo leo
Asubuhi Katika Eneo la Nyaugao Mpakani Mwa Kijiji cha Makoga na Mdasi.
Kona
Iliyosababisha Ajali ya Mmoja Kufariki na Wengine Wawili Kujeruhiwa
Vibaya na Kukimbizwa Katika Hospitali ya Ikonda Makete leo Asubuhi Huko
Mdasi Wanging'ombe.
Naibu Waziri
wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge akiwasili eneo la Tukio Hilo ambako
alitakiwa Kufanya Mkutano na Wapiga Kura wake na Kisha Kulazimika
kuahirisha Mkutano Huo.
Hapa Mbunge
Lwenge akitoa Pole katika Msiba Huo na rambi rambi ya Tshs.Laki Moja
Barabarani Ulipotokea Msiba kabla ya Jeshi la Polisi Kuwasili Eneo Hilo.
Na Gabriel Kilamlya.
Mtu Mmoja Amefariki Dunia na Wengine Wawili Wamejeruhiwa Katika Ajali ya Pikipiki Iliotokea Leo Asubuhi Katika Kijiji Cha Mdasi Kata ya Makoga Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe.
Wakizungumza na Mwandishi wetu Baadhi ya Mashuhuda wa Ajali Hiyo Akiwemo Diwani wa Kata ya Makoga Bw Abraham Chaula Amesema Ajali Hiyo Imetokea Leo Katika Barabara Kuu ya Njombe - Makete.
Amemtaja Mtu Aliefariki Kwenye Ajali Hiyo Kuwa ni Linus Nziku Mkazi wa Kijiji Cha Mdasi na Kusema Kuwa Majeruhi Wawili Wamekimbizwa Katika hospitali ya Ikonda Kwa Matibabu Zaidi.
Aidha Pamoja na Kuelezea Mazingira ya Tukio Hilo,Bw Chaula Amewashauri Watumiaji wa Vyombo Vya Usafiri Hasa Pikipiki Kuwa Makini Wanapokuwa Barabarani.
Jeshi la Polisi Limethibitisha Kutokea Kwa Tukio Hilo.