MWANGALIE KIJANA ALIYERUDISHWA KUTOKA MSUKULENI JUMAPILI

Ushuhuda wa kijana aliyerudishwa kutoka msukuleni siku ya jumapili ya juzi katika ibada iliyofanyika kanisa la Ufufuo na Uzima Morogoro. 

Ushuhuda huu GK imeupata kupitia moja ya kurasa za Facebook zinazomilikiwa na kanisa la Ufufuo na Uzima nchini.

Ni mara baada ya somo zuri lililofundishwa na Mchungaji Kiongozi Dr Godson Issa Zacharia lenye kichwa kinachoitwa MATUKIO YA KICHAWI, yakifuatia maombi yaliyojaa uwezo wa Roho Mtakatifu ambayo yalipenya hadi kumkuta huyu kijana akiwa kwenye vifungo vya shetani. na mara baada ya kurudishwa kijana huyo toka msukuleni alihojiwa na kuelezea kuwa alichukuliwa msukule na bibi yake na mara baada ya kuchukuliwa alilazimishwa kumeza hirizi tatu na kijiti kimoja ambacho kilikaa kwenye koo lake hali ambayo ilimfanya kijana huyo ashindwe kumeza,

na alipoulizwa na mchungaji Godson kuwa alikuwa amewekwa wapi? kijana huyo alijibu kuwa alipelekwa mtwara na alikuwa anafanyishwa kazi ya kuvua samaki kwa muda mrefu. na mara baada ya kuitwa NJOOOOOOOO akajikuta yupo kanisani na anasema amewaacha na wenzake wengine huko. Baada ya hapo kijana huyo alipewa maji ya kunywa akanywa yote bila shida.

MUNGU WETU NI MUNGU WA KUOKOA NA NJIA ZA KUTOKA MAUTINI ZINA YEYE. 
 
CHANZO: GK


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo