MWANAUME AFUMWA AKIFANYA MAPENZI NA KUKU!

Kuku
MWANAMUME anazuiliwa katika kituo kimoja cha polisi mjini Nyeri nchini Kenya baada ya kufumaniwa akifanya mapenzi na kuku.
Mwanamume huyo mwenye umri wa zaidi ya miaka 50 alikamatwa Alhamisi jioni baada ya kupatikana akifanya kitendo hicho katika kijiji cha Kigwandi, wilaya ya Tetu.

Kaimu afisa mkuu wa polisi katika eneo hilo, Bw Joseph Mwika alisema mwanawe mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 10 alimuarifu kakake mkubwa baada ya kumfumania babake akifanya kitendo hicho.

Bw Mwika alisema wawili hao walimripoti baba yao kwa chifu wa eneo hilo ambaye alimkamata na kumpeleka katika kituo cha polisi.

“Kuku huyo alikuwa wa mwanawe mwanamume huyo aliyeripoti kisa hicho kwa chifu,” alisema Bw Mwika.

Kuku huyo ambaye baadaye alikufa alipelekwa katika maabara ili kufanyiwa uchunguzi.

“Tunasubiri matokeo ya madaktari wa mifugo kabla ya kuchukua hatua,” afisa huyo alisema.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo