HII NI SIKU RAY C ATAKAYOANZA RASMI MUZIKI BAADA YA KUUMWA

Mabibi na mabwana mko tayari kwa ujio mwingine wa Ray- C. Malkia wa kiuno bila mfupa Rehema Chalamila aka Ray-C ametangaza ujio wake rasmi baada ya kuwa chimbo kwa kipindi kirefu toka apate matatizo miezi kadhaa iliyopita. Ni baada ya siku chache kupita toka Ray-C atamke kuwa anapenda sauti ya ‘dogo lake’ Recho na kuwa atakuja kufanya naye kazi, leo amethibitisha kuwa mwezi Agosti ndio anarudi rasmi kutoka chimboni.

Kupitia akaunti ya Instagram Ray-C aliweka picha ya gazeti moja lililoandika ‘Ray-C kuonekana hadharani mwezi Agosti’, na baada ya followers wake kutaka ufafanuzi ndipo alifunguka kwa kusema “For Sure it’s bout time nw nimewapa muda sana watoto sasa mdada is coming back”.
Ray C aliwauliza marafiki zake wa Instagram kama wapo tayari kwa ‘come back’ yake, wengi wameonekana kutamani muda ufike waweze kumuona tena Ray-C akirudi katika muziki.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo